Saturday, January 30, 2010

Changa Moto... Poem by the first group of Zanzibits students 2010

I was very happy and surprised with the student of lot one in the morning when they presented a poem. It is in kiswahili, but it's very nice, so I thought it would be nice to publish here on the blog.

This is just the start, as we are going translating the text to english and we will make a special song for Zanzibits, as some of our stutents are real singing artitst, this year :)

ASHA
Tunaanza na salamu,
Kwa zanzibits walimu,
Assalam-alaykumu,
Muwaje hali zenu.

SAID
Tumepania kurudi tena,
Wasichana na wavulana,
Mie nahisi hakuna namna,
Kozi two tutakutana.

ZAINA
Vizuri tuliisongesha,
Class tukaipaisha,
Performance tukaimarisha,
Walimu vipi mnabisha?

RAHMA
Pamoja tulishirikiana,
Kama timu ya madizaina,
Hatukusita kukosoana,
Vizuri tukasaidiana.

RAYA
Ilikuwa ni kama sapraizi,
Ndani ya wiki nne za kozi,
Tumeimaliza kazi,
Ingawa ni overdozi.

ASHA
Hizi ni zenu salamu,
Group B mfahamu,
Sasa ni yenu awamu
Mtaweza kuperformu?

ABDUL-RAHMAN
Wanafunzi nauliza
Hatuwezi tunaweza?
Au mi nnajikweza?
Kwa pamoja… ‘tunawezaaa’

Poem by Said.

Great work, guys! Keep up the good vibe and enjoy your weekend.

Guy

No comments: